Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndugu Mussa Kitungi amewataka wasimamizi wa miradi kuongeza umakini katika kusimamia miradi inayotekelezwa ili iweze kukamilika kwa wakati.
Ndugu Kitungi ametoa maelekezo hayo Agosti 20, 2025 wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya elimu ambapo aliambatana na baadhi ya Wakuu wa Divisheni na Vitengo.
Ameeleza kuwa ni muhimu kutekeleza miradi kwa wakati pamoja na kuzingatia thamani ya fedha ili wananchi waanze kunufaika na miradi hiyo.
" Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan analeta fedha nyingi sana kwa ajili ya miradi, hivyo hatutaruhusu myu yeyote atukwamishe bila kumchukulia hatua. Ongezeni juhudi na umakini katika usimamizi wenu na kwenye changamoto msisite kusema ili miradi yetu ikamilike vile ilivyokusudiwa" alieleza.
Ndugu Kitungi alipata fursa ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Jimbo katika kata ya Kirongwe, mradi wa ujenzi wa shule ya msingi katika kitongoji cha Mwawani, ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule ya msingi Kungwi kata ya Baleni, ujenzi wa maabara ya kemia na baiolojia shule ya sekondari Kidawendui katika kata ya Ndagoni pamoja na ujenzi wa shule ya Amali iliyopo kijiji cha Dongo.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.