" Mnalo jukumu kubwa la kudumisha muungano wetu" asema Mhe. Aziza Mangosongo, Mkuu wa Wilaya ya Mafia wakati wa Kongamano la Vijana la Miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililofanyika leo Aprili 26, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri.
Kongamano hilo lililoratibiwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Idara ya Elimu Sekondari, limehusisha vijana kutoka shule ya Sekondari ya Kilindoni pamoja na chuo cha ufundi VETA.
Mhe. Mangosongo ameeleza kuwa miongoni mwa mambo yanayotuunganisha ni pamoja na ulinzi na usalama, hivyo hatuna budi kuhakikisha tunawajibika kutunza amani iliyopo.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia Ndugu Shabani Shabani amewaasa vijana kujitoa kizalendo ili kuleta maendeleo katika Taifa.
"Ili nchi yetu iende vizuri, inabidi software (akili) ifanye kazi vizuri kwa manufaa ya nchi" alisema Ndugu Shabani akisisitiza kwamba kwa kufanya hivyo watakuwa wanaenzi mazuri yote ya waasisi wa nchi.
Aidha, amewaasa vijana kutorubunika na kuhakikisha wale wote ambao hawakujiandikisha, wanatumia haki yao ya msingi kujiandikisha katika daftari la kudumu mara zoezi hilo litakapoanza kwa mara ya pili ili waweze kupiga kura katika uchaguzi mkuu 2025.
Mada mbalimbali zilitolewa ikiwemo uzalendo, mapambano dhidi ya UKIMWI na Ukatili wa kijinsia, matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii, kuepuka vitendo vya utovu wa nidhamu, kama matumizi ya dawa za kulevya, na vitendo vingine vya kuvunja sheria.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka huu ni " Muungano Wetu ni Fhamana, Heshima na Tunu ya Taifa, Shiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
" Hapo mwanzo nilikuwa nikitumia sana kuni na mkaa, ila baada ya kushiriki mafunzo kuhusu matumizi ya jiko la nishati safi, nitakuwa wa kwanza kuhamasisha wenzangu kutumia nishati safi hasa kwa wachakataji wa samaki, mama lishe wenzangu na wengine" alisema Bi. Aisha Salum, mjasiriamali kutoka kata ya Kilindoni.
Hapo awali, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Juma Salum alitoa wito kwa wafanyabiashara kutumia fursa hiyo ili kutumia teknolojia mpya ya nishati ya kupikia na kuachana na matumizi ya kuni ambayo yamekuwa si rafiki kwa mazingira.
Majiko hayo yanayotumia mkaa utokanao na mabaki ya vifuu vya nazi, machicha na makumbi ya nazi na mabaki mbalimbali ya mazao ya shambani, yanatarajiwa kuuzwa kwa bei ya punguzo kutoka Shilingi 125,000 hadi kufikia Shilingi 35,000 kwa wakazi wa Mafia, na baadhi ya majiko yatatolewa bure kama mfano.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.