Halmashauri imetoa jumla ya Tshs 97,700,000 kwa vikundi 08 vya wanawake ( Tshs 51,000,000) , vikundi 04 vya vijana (tshs. 45,500,000) na mlemavu mmoja tshs 1,200,000. Fedha hizo zimetokana na marejesho ya mkopo wa 10% inayotolewaga kwa vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu. Vijiji vilivyonufaika ni pamoja na
Jojo, Jimbo, Kirongwe, Ndagoni, Kilindoni na Kiegeani.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mhandisi Martin Ntemo Mkuu wa Wilaya Mafia alisisitiza kuwafichua watu wanaowatumia wanavikundi ili kujinufaisha binafsi.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Juma Salum ambaye aliambatana na mgeni rasmi alihimiza wana vikundi wanaopewa fedha za mikopo warejeshe kwa wakati na kuwa marejesho yanapofanywa kwa wakati inatoa fursa kwa wakopaji wengine ambapo kwa mwaka jana 2021/2022 Halmashauri ilikuwa ya 8 Kitaifa kwa utoaji wa mikopo na hii ilitokana na marejesho mazuri kwa wakopaji.
Kwa upande wa meneja wa NMB na CRDB ambao pia walihudhuria hafla hiyo walisisitiza kutumia akaunti zao kwani hazina makato ya mwezi na wakati wa utoaji fedha ni bure.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.