Viongozi wa dini pamoja na viongozi wa asasi za kiraia wapewa wito kuhamasisha jamii kujitokeza kuboresha taarifa katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Wito huo umetolewa leo Mei 9, 2025 na Afisa Mwandikishaji wa Wilaya ya Mafia Ndugu Mohammed Othman wakati wa kikao na viongozi hao katika ukumbi wa Halmashauri uliopo Chicco.
Hilo linajiri wakati ambao zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa awamu ya pili na ya mwisho linatarajiwa kuanza ifikapo Mei 16, 2025 wilayani Mafia ambapo zoezi litaendeshwa kwa siku 7 hadi tarehe 22 Mei, 2025.
Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura utafanyika katika vituo 15 wilayani Mafia na kuwapa fursa wananchi wenye sifa ambao hawakuweza kuboresha taarifa zao wakati wa awamu ya kwanza ya zoezi hilo.
"Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora ".
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.