Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mwl. Kassim Ndumbo amewataka viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Dongo kuweka jitihada kubwa katika kutatua kero za wananchi kijijini hapo.
Mwl. Ndumbo ametoa maagizo hayo wakati wa kikao chake na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Dongo alipokuwa akisikiliza kero zao pamoja na kupanga mikakati ya utatuzi wa kero hizo.
"Mapato ya kijiji yatumike kusaidia kutatua changamoto za wananchi kulingana na kiasi kinachokusanywa, ili wote kwa nafasi zetu tupambanie maendeleo ya wilaya yetu na nchi kwa ujumla" alisema Ndumbo.
Akiwa ameambatana na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri, Mwl. Ndumbo alipata nafasi ya kusikiliza kero za baadhi ya wananchi wa kijiji cha Dongo ambao walipongeza jitihada za Serikali katika kuleta miradi ya maendeleo na kuiomba Serikali kuendelea kutatua kero zao ikiwemo upungufu wa walimu pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara.
" Naishukuru Serikali kwa kutuletea miradi ya maendeleo kijijini kwetu lakini tunaomba itusaidie kuongeza idadi ya walimu katika shule yetu ya msingi ya Sikula pamoja na kutuboreshea barabara" alisema Hassan Hamsini, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Sikula.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji aliwapongeza viongozi wa Serikali ya Kijiji kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo iliyopo kijijini hapo, hasa mradi wa Shule Mpya ya Msingi ya Sikula na kuwataka wafanye kila linalowezekana kutatua changamoto zinazokwamisha miradi.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.