Viongozi wateule wa serikali za mitaa wametakiwa kuzingatia uadilifu na kujituma katika kazi ili kukiishi kiapo walichoweka.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo, Desemba 2, 2024 wakati wa zoezi la kuapishwa viongozi hao wakiwemo Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji, Wajumbe Mchanganyiko na Wajumbe kundi la Wanawake.
Mhe. Mangosongo amewataka viongozi hao kutenda haki kwa kuwatambua wananchi ambao wapo katika makundi maalum wakiwemo walemavu na wazee pamoja na kutatua migogoro mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardhi na kuzuia uvunjifu wa sheria kama uvuvi haramu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndugu Mussa Kitungi amewaasa viongozi hao kujitoa katika uongozi wao ili waweze kuwatumikia vizuri wananchi kwa kusimamia vizuri miradi na mambo mbalimbali ya kimaendeleo.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.