Wizara ya Katiba na Sheria leo Machi 13 imeongoza mafunzo kwa baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, wajumbe wa Kamati ya Usalama pamoja na Maafisa Watendaji Kata.
Mafunzo hayo yahusuyo Uraia na Utawala Bora yamelenga kuwajengea uwezo maafisa hao kuhusu haki na wajibu wao kikatiba ili waweze kuboresha utendaji kazi katika majukumu yao ya kila siku.
Akielezea matarajio ya wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Uongozi wa Mkoa wa Pwani na Wilaya, Mratibu wa Mafunzo hayo Ndugu Prosper Alexander ameeleza kuwa wana imani kuwa waliyoyafundisha yataenda kutekelezwa.
" Tunatarajia kwamba tutaona mabadiliko makubwa kwenye jamii, na kwamba mafunzo waliyoyapata, wataenda kuyashusha chini kwa wasaidizi wao ili kuboresha utendaji kazi" alisema Ndugu Alexander.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.