Afisa Mwandishikishaji wa Jimbo la Mafia Ndugu Mohamed Othman amewataka Maafisa Waandikishaji Wasaidizi pamoja na Waendesha Vifaa vya Bayometriki kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu mkubwa pamoja na kuzingatia miongozo na sheria ili kufanikisha zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa awamu ya pili.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Waandikishaji Wasaidizi na Waendesha vifaa vya bayometriki yaliyofanyika Mei 14, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri, Ndugu Othman amesisitiza juu ya umuhimu wa kuwajibika ipasavyo pamoja na kujituma ili kuepusha kero kwa wananchi.
" Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewaamini tena na kuwapa jukumu hili kwa awamu ya pili kutokana na kazi nzuri iliyofanyika katika awamu ya kwanza, hivyo ni matumaini yetu kwamba mtazingatia mafunzo haya na kwenda kuwajibika ipasavyo kwa kuzingatia sheria na miongozo muwapo vituoni" alisema Ndugu Othman.
Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura linatarajiwa kufanyika kwa siku saba kuanzia Mei 16 hadi 22, 2025 katika vituo 15 wilayani.
" Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora".
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.