Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia leo Februari 10, 2025 wamepata mafunzo pamoja na kula kiapo cha kujitoa uanachama wa Chama cha siasa.
Akifungua mafunzo hayo, Afisa Mwandishikishaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndg. Mohammed Hussein amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa waadilifu ili zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura lifanyike kwa amani na utulivu na kwa ufanisi mkubwa.
Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linatarajiwa kuanza Februari 13, na kumalizika Februari 19, 2025 ambapo vituo vyote 73 vilivyopo wilayani vitakuwa vinafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.