Wataalam kutoka Shirika la World Fish wakishirikiana na Kitengo cha Uthibiti Ubora wa Mazao ya Uvuvi cha Wizara ya Mifugo na Uvuvi wamefika wilayani Mafia kwa lengo la kuona na kukagua eneo lililotolewa na Serikali ya Kijiji cha Chunguruma kilichopo kata ya Ndagoni kwa ajili ya mradi wa kuchakata dagaa.
Mradi huo unaofadhiliwa na FCDO, unatarajiwa kuongeza thamani na ubora kwa ajili ya kuongeza usalama kwa walaji huku ukitunza mazingira kwa kuzingatia matumizi ya nishati safi, na kukuza soko la dagaa kimataifa ambalo kwa sasa, soko kubwa lipo nchi ya Kongo.
Eneo la ukubwa wa Hekari sita limetengwa na Serikali ya Kijiji kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.