Taasisi ya Kalamu Education Foundation ( KEF) imetoa msaada wa Kilo 1500 za chakula ikiwemo Kilo 1000 za mchele, kilo 500 za maharage, lita 100 ya mafuta, Katoni 30 za karatasi (Rim) pamoja na wino kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopo kambini wilayani Mafia.
Akipokea msaada huo katika shule ya Sekondari Micheni Septemba 25, 2024, Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ametambua na kupongeza jitihada za taasisi hiyo kuendelea kuiunga mkono Serikali katika masuala ya elimu wilayani na kutoa wito kwa taasisi nyingine kushirikiana na Serikali kuboresha elimu.
" Tuna taasisi nyingi sana Tanzania, ila hawa ni miongoni mwa taasisi ambazo zipo hai, tunawashukuru kwa kuiunga mkono Serikali ili kuboresha elimu"
Aidha, Mhe. Mangosongo amewataka wanafunzi kuongeza jitihada katika masomo ili wapate matokeo mazuri.
Utaratibu wa kuandaa kambi za wanafunzi ulianza mwaka 2020, ambapo shule ya Sekondari Micheni ni miongoni mwa shule tatu ambazo ni kambi kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha nne wilayani Mafia ambao wanajiandaa na mitihani ya Taifa. Kambi nyingine ni Shule za Sekondari Kirongwe na Bweni ambazo kwa ujumla zote zina wanafunzi 705 wa kidato cha nne.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.