Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo amehitimisha mafunzo kwa washiriki 19 wilayani Mafia.
Mafunzo hayo yaliyoongozwa na Chuo cha Taifa cha Utalii yalihusisha wadau waliopo katika mnyororo wa utalii ambao wamejifunza kuhusu utengenezaji wa bidhaa za utalii, uboreshaji, uongezaji wa thamani na kuzitangaza bidhaa zao katika masoko; ndani na nje ya nchi.
Mhe. Mangosongo amelishkuru Shirika la WWF kwa mchango wao kudhamini mafunzo hayo na kutoa wito kwa wadau hasa wataalam wa masuala ya utalii kuendelea kutoa elimu juu ya shughuli zinazohusu utalii, uongezaji wa thamani katika bidhaa pamoja na uhifadhi wa mazingira.
Aidha, amewataka wafanyabiashara kutumia fursa zilizopo ikiwemo kujitangaza zaidi na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa majukwaa mbalimbali ili waweze kuonesha bidhaa na kazi zao.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.