Shirika linalojihusisha na Uhifadhi wa Mazingira na Utunzaji wa Papa Potwe wilayani Mafia ( WATONET) leo Februari 25, 2025 limeongoza warsha kwa kukutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wadau wa utalii na mazingira.
Warsha hiyo ina lengo la kutoa motisha Kwa jamii na wadau wa uhifadhi wa utalii wa Papapotwe kushiriki katika masuala ya uhifadhi wa rasilimali za Bahari Kwa manufaa ya kizazi Cha sasa na badae.
Kwa kukutanisha Taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Bodi ya Watalii Tanzania (TTB), Hifadhi ya Bahari Mafia, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania ( TAFIRI), pamoja na taasisi zisizo za kiserikali ikiwemo taasisi ya Kilimo Endelevu kutoka Zanzibar, pamoja na vyama vya kijamii kama Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Bahari na Fukwe ( BMU), wachakataji wa mazao ya bahari, viongozi wa Chama cha Wavuvi, wavuvi, pamoja na baadhi ya wamiliki wa hoteli, warsha hiyo inatoa fursa ya wadau kushirikishwa katika masuala ya msingi yatakayosaidia kukuza sekta ya utalii, uvuvi na uhifadhi.
Warsha hiyo inayofadhiliwa na shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF), inatarajiwa kuhitimishwa kesho Februari 26, 2025 kwa wadau kuandaa mapendekezo ya mpango kazi utakaosaidia mgawanyo wa manufaa na mbinu ya uhifadhi yenye motisha.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.