Wananchi kutoka Utende na Chole wameshiriki katika mradi wa kufikisha umeme kisiwani Chole kwa kuzamisha waya ndani ya maji kutoka fukwe za Utende hadi fukwe za Chole.
Mradi huo wa Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania( TANESCO), umetekelezwa katika sehemu tofauti ambapo ullihusisha umeme wenye msongo mkubwa wa KV 11 kwa kuvuta nguzo Mita 300 na uwekaji wa waya wenye urefu wa Kilomita 1.3 na ukubwa wa Milimita 95.
Waya unaozamishwa ndani ya maji ambao pia unabeba nyuzi za kupitisha mawasiliano na kuwezesha mtandao kupatikana kisiwa cha Chole, una uwezo wa kubeba umeme wa msongo wa KV 33, lakini kwa sasa umeme utakaowekwa ni wa KV 11, endapo Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania ( TANESCO) wakiongeza uwezo wa msongo wa umeme, waya huo utaendelea kubeba umeme wa msongo mkubwa.
Mradi huo unatarajiwa kuleta maendeleo makubwa kiuchumi kwa kutoa fursa kwa wakazi wa kisiwa cha Chole kujihusisha na shughuli nyingi zinazohitaji umeme, hasa kwa wafanyabiashara wa samaki pamoja na kuboresha utoaji wa huduma za afya.
" Mradi huu ulikuwa wa miezi tisa, sasa umefikia hatua za mwisho, japo tulichelewa kupata kibali cha kuvusha waya baharini, sasa tumekipata na tunahakikisha kwamba ndani ya wiki mbili, umeme utakuwa umewaka katika kisiwa cha Chole" alieleza Celestine Igongo, meneja wa miradi kutoka Nakuroi Investment, kampuni iliyopewa zabuni ya utekelezaji wa mradi.
Vijiji vingine ambavyo ni Juani na Jibondo, vitanufaika na upatikanaji wa umeme baada ya kumalizika kwa zoezi hilo katika kisiwa cha Chole.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.