Shirika lisilokua la kiserikali linajulikana kwa jina la Kalamu Education Foundation (KEF) limetoa msaada wa chakula kwa wanafunzi wa kidato cha nne wanaojiandaa na mtihani wa Taifa wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2022.
Wametoa unga wa mahindi kg 2,700 na maharage kg 1,400.
Wakati wa hafla ya kukabidhi vyakula hivyo wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri na KEF walipata wasaa wa kuongea na wanafunzi hao kuwatia moyo na kuwapa hamasa ya kufanya vizuri wakiwaasa wazingatie mambo makuu matano yakiwemo 1. Mungu kwanza 2. kujiamini 3. kusoma kwa bidii 4. Nidhamu 2. kulenga wanataka kuwa nani
Mkurugenzi Mtendaji (W) Bw. Kassim S. Ndumbo aliwashukuru sana KEF kwa moyo wao wa uzalendo na kuwapenda watu wa Mafia kwani wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali kwa shule na wanafunzi, na hata walipoelezwa kuna uhaba wa chakula kwa wanafunzi waliopo kambi waliahidi kufanya chochote na hatimaye kutimiza ahadi yao.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.