Halmashauri ya Wilaya ya Mafia kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali washiriki usafi wa fukwe kwa kuokota plastiki katika eneo la Bondeni pwani.
Zoezi hilo limeratibiwa na Jukwaa la Mabadiliko ya tabianchi ( FORUMCC) na Shurika la Kimataifa la Kuhifadhi mazingira (IUCN) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, taasisi za Kiserikali na zisizo za kiserikali zikiwemo Hifadhi ya Bahari Mafia, WWF, Wakala ya Misitu Mafia, Takataka Dampo ,vikundi mbalimbali vya jamii na wananchi wa eneo la Bondeni Pwani.
Wananchi zaidi ya 250 walishiriki zoezi hilo ambapo jumla ya chupa za plastiki zaidi ya 674 za vinywaji tofauti ziliokotwa.
Zoezi hilo limeongozwa na kauli mbiu isemayo " Badili Tabia, Kataa Matumizi Holela ya Plastiki".
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.