Katibu Tawala Wilaya ya Mafia Ndugu Shabani Shabani amekutana na vikundi vya wajasiriamali vya kata ya Kilindoni vilivyopatiwa Mikopo ya asilimia 10 ya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu.
Akizungumza na wanufaika hao Machi 11, 2025, amewaomba waendelee kumuunga mkono Mhe. Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mabalozi wazuri katika jamii kusambaza elimu waliyoipata ya namna bora ya kutumia mikopo hiyo kujiinua kiuchumi.
Aidha, amewataka kuitumia mikopo hiyo kwa kazi ilivyokusudiwa ili waweze kufanya marejesho katika mpango mzuri na uaminifu.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.