Kamati ya Usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo, leo Januari 07, 2025 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali wilayani ikiwemo afya, elimu, miundombinu ya maji na barabara.
Katika ziara hiyo, Mhe. Mangosongo amewataka wasimamizi wa miradi kuongeza kasi ya utekelezaji ili miradi ikamilike kwa wakati uliokusudiwa pamoja na kuzingatia taratibu na miongozo iliyopo ya usimamizi wa miradi.
Aidha, amezitaka taasisi zote zenye miradi wilayani pamoja na Halmashauri kuhakikisha kwamba thamani ya miradi inaendana na fedha ambazo Serikali imetoa kwa ajili ya utekelezaji.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Kichangachui-Msufini, ujenzi wa Zahanati za Micheni na Kibada katika kata za Miburani na Baleni, ujenzi wa kalvati kubwa la midomo miwili katika barabara ya Kibaoni- Chemchem, ujenzi wa bweni lililopo shule ya sekondari Kilindoni, mradi wa maji katika kata ya Baleni, pamoja na ujenzi wa kalvati lililopo Jimbo, kata ya Kirongwe.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.