Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndg. Mussa Kitungi akiwa katika kikao na Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. Shabani Shabani, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Fedha, Kituo cha Ubia baina ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma ( PPPC).
Lengo la ziara ya wataalam hao ni kujengeana uwezo na kuibua miradi inayoweza kuendeshwa kwa UBIA baina ya sekta ya Umma na sekta Binafsi.
Moja ya vigezo vya miradi hiyo ni kuwa miradi yenye vivutio vya kibiashara ili kuweza kuwavutia wawekezaji, na baada ya kuibua miradi hiyo na kujiridhisha kuwa Halmashauri ina umiliki halali wa maeneo hayo, miradi itatangazwa Kwa ajili ya kuwaalika wawekezaji kuja na kuwekeza.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.