Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndugu Mussa Kitungi amewaongoza watumishi pamoja na wananchi wa Kitongoji cha Mwawani kiliopo kijiji cha Kifinge, kata ya Baleni katika zoezi la hamasa ya ushiriki wa ujenzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Mkondo Mmoja pamoja na nyumba ya watumishi.
Zoezi hilo lililofanyika Julai 12, 2025 limeratibiwa na Idara ya Elimu Msingi kwa kushirikiana na Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali kutoka Halmashauri.
Ndugu Kitungi ametoa pongezi kwa watumishi, Serikali ya Kijiji cha Kifinge pamoja na wananchi wote kwa kushiriki katika zoezi hilo na kutoa wito kwa wananchi kujitoa kuchangia nguvu zao ili mradi uweze kukamilika kwa wakati na kuondoa adha kwa wanafunzi wanaolazimika kutembea umbali mrefu kuifuata shule.
Aidha, amesisitiza usimamizi bora wa miradi yote inayotekelezwa wilayani ili utekelezaji wa miradi hiyo uendane na thamani ya fedha ambayo Serikali inatoa ili wananchi wapate huduma iliyo bora.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.