Watumishi wilayani Mafia wameshiriki matembezi ya hisani kwa lengo la kumpongeza na kumshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zote anszozifanya katika kuhakikisha nchi inapata maendeleo pamoja na kuwajali watumishi wa umma.
Wakiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. Shabani Shabani, watumishi waliungana na baadhi ya wananchi kutoa pongezi na shukrani zao pamoja na kutoa tamko lao kwa pamoja.
"Awamu hii imekuwa ya faraja, furaha na matumaini kutokana na ushirikiano tunaopata kutoka kwa Serikali yetu. Hivyo hafla hii ya kumpongeza Mhe. Rais ni jambo la shukrani na uungwana kwetu na si la kisiasa" alieleza Ndg. Shabani
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewapongeza watumishi kwa hatua hiyo pamoja na kueleza mambo muhimu ambayo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameyatekeleza Wilayani Mafia na kuwataka watumishi kuongeza juhudi katika kazi ili wananchi wapate huduma bora.
Kwa sasa, Halmashauri ya Wilaya ya Mafia ina watumishi asilimia 70 ya watumishi wote wanaohitajika, hii ni kutokana na jitihada kubwa ya Mhe. Rais kuongeza watumishi ambapo miaka ya nyuma uhaba ya watumishi ulikuwa mkubwa zaidi.
Miongoni mwa mengi ambayo Mhe. Rais ameyafanya ni pamoja na kupunguza kodi kwenye mishahara, kupanda madaraja, kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo, kuboresha masuala ya kitumishi kwa kuwa na mfumo wa Serikali mtandao ambao unaoongeza ufanisi, kupanda kwa mishahara, na kuwezesha mafunzo kazini ambapo mambo haya yamekutanisha wananchi kutoa pongezi kwa Serikali.
Aidha, kwa pamoja watumishi wameahidi kufuata maelekezo na miongozo ya Serikali, kuongeza juhudi katika kutumikia wananchi, kuunga mkono jitihada za kutunza mazingira pamoja na mambo mengine ambayo yanasaidia kuchangia maendeleo ya Wilaya na Taifa kwa ujumla.
Matembezi hayo yalifuatiwa na shughuli nyingine za uchangiaji wa damu pamoja na mchezo wa mpira wa miguu ambapo timu ya watumishi ilishindana na timu ya waendesha bodaboda.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.