Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo (MB) amewaagiza watendaji wa serikali mkoani Pwani kuondoa urasimu unaokwamisha juhudi za Rais Samia Suluhu Hassani za kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza katika mkoa huo.
Ametoa agizo hilo mkoani Pwani wakati wa kongamano la uwekezaji lililofanyika katika shule ya uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo mjini Kibaha.
Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha kwamba juhudi zinazofanywa na Rais Samia kuvutia uwekezaji nchini hazikwamishwi na wawekezaji waokuja kuwekeza hawakwamishwi na changamoto yoyote.
Amesema serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji kwa kuimarisha miundombinu muhimu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Amewahakikishia wawekezaji wote wanaotaka kuja kuwekeza nchini kuwa Tanzania ni sehemu salama kwa uwekezaji kutokana amani na utulivu iliyopo
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhe. Abubakari Kunenge amesema hali ya uwekezaji katika mkoa wa Pwani imezidi kuongezeka na wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza mkoa wa Pwani kwani serikali imeweka na inaendelea kuweka miundombinu bora barabara, nishati ya umeme na huduma nyingine zinaendelea kuboreshwa
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.