Timu ya wataalam kutoka Wizara ya Afya kupitia mradi wa Global Fund, leo Mei 13, 2025 imefanya ufuatiliaji wa shughuli za miradi zinazotekelezwa wilayani Mafia.
Lengo la ziara hiyo ni kuboresha mifumo ya huduma za afya ili kuwezesha jamii kupata huduma bora hususani katika kudhibiti magonjwa ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria.
Miradi iliyotembelewa ni kichomea taka ( incinerator) pamoja na mitambo ya kuzalisha Hewa Tiba ( PSA Oxygen Plant) iliyopo katika Hospitali ya Wilaya.
Miradi hiyo inayotekelezwa wilayani hapo ina faida kubwa kwa wananchi kwa kuhakikisha kuwa taka zinazozalishwa katika Hospitali ya Wilaya na Vituo vya Afya vya jirani zinateketezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kichomea taka.
Aidha, mradi wa mitambo ya kuzalisha hewa tiba utasaidia kina mama wajawazito, wagonjwa mahututi na wagonjwa wengine wanaolazimika kufanyiwa upasuaji.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.