Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani ( WWF) leo Februari 24, 2025 limekabidhi vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni 109 kwa vikundi 12 vinavyojishughulisha na kilimo cha mwani kutoka vijiji vya Jimbo na Kanga.
Hatua hiyo ni muhimu katika kuhakikisha kuwa kuna ongezeko la thamani katika zao la mwani kwa kuinua hali ya uchumi kwa wakulima wa zao hilo pamoja na kuweka kipaumbele katika utunzaji wa mazingira kwa kurejesha mikoko.
Akikabidhi vifaa hivyo, Msimamizi wa miradi ya huduma ndogo za kifedha kutoka WWF, James Golola, ameiomba Halmashauri kupitia Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuweka usimamizi mzuri kwa vikundi hivyo ili waweze kutunza na kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokisudiwa.
Shirika la WWF linatekeleza mradi wa "NORAD MANGROVE" kwa kushirikisha jamii ili uhifadhi wa mazingira uwe endelevu na kunufaisha jamii husika kwa kuwawezesha kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.