hirika linalojihusisha na Uhifadhi wa Mazingira Duniani ( WWF) limekabidhi boti na pikipiki ( Toyo) mbili zenye thamani ya Shilingi Milioni 57.5 kwa vikundi viwili vya urejeshaji wa mikoko kutoka vijiji vya Kanga na Jimbo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo leo Juni 27, 2025 Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe .Aziza Mangosongo amelishukuru shirika la WWF kwa ushirikiano wao kwa Serikali na jamii kiujumla katika kuunga mkono juhudi za utunzaji wa mazingira ili kukomboa rasilimali zilizopo katika kisiwa cha Mafia na kueleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na mashirika na wadau ili kutunza mazingira na kusaidia kuleta maendeleo katika jamii.
" WWF mmeona mtushike mkono Serikali, na sisi tunashukuru kwa dhati ila tunawaomba ndugu zetu mnaopokea vifaa hivi kwamba mvitumie kwa lengo lililokusudiwa" alieleza Mhe. Mangosongo.
Wanufaika wa vikundi hivyo wamepongeza hatua hiyo na kuahidi kuvitunza vifaa ili viwasaidie katika kuendelea kutunza rasilimali zilizopo pamoja na shughuli zao za kuwaingizia kipati hasa ukulima wa mwani.
" Tunaishukuru WWF na viongozi wetu kwa kuendelea kutusaidia katika shughuli zetu, tunaahidi kutumia kwa matumizi sahihi vifaa vyetu ili viweze kutunufaisha sisi kama kikundi na kuhifadhi mazingira yetu" alisema Amini Jumbe, mwanakikundi kutoka Umoja wa Mwani Jimbo.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.