Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia alitoa motisha kwa walimu wote wa sekondari wa wilaya ya Mafia pamoja na watumishi waliopo ofisi ya Afisa Elimu sekondari kwenda kufanya utalii wa kutembelea hifadhi ya taifa ya Ngorongoro mkoani Arusha. Katika safari hiyo waliambatana na diwani ambaye pia ni Mwenyekiti wa huduma za kijamii Mheshimiwa Hassan M. Hassan na Bw. Silvanus Kunambi kutoka ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Pwani.
Motisha hiyo waliipata baada ya kufanya kazi kubwa kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2020 baada ya kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia 88.9 kutoka asilimia 67 ya mwaka 2019.
Katika safari hiyo walipata pia fursa ya kutembelea shule ya sekondari Lugoba iliyopo Wilayani Chalinze na shule ya sekondari Welwel iliyopo wilayani Karatu Mkoa wa Arusha.
Wakiwa katika shule ya sekondari Welwel walipata nafasi ya kubadilishana uzoefu na walimu wenzao.
Pia walitembelea Hifadhi ya Taifa ya za wanyama Ngorongoro ambapo walipata fursa ya kutembelea familia moja ya wamasai waishio ndani ya hifadhi hiyo ambapo waliona na kujifunza mila na desturi mbalimbali za kabila la wamasai.
Katika hifadhi hiyo ya Ngorongoro walipata bahati ya kuona wanyama wengi wakiwemo Nyati, Tembo, Vifaru, Simba, Swala na wengineo wengi.
Walimu hao waliifurahia sana safari hiyo ambayo walisema iliwapa motisha na ari ya kufanya kazi kwa bidii za zaidi na ikiwezekana kwa mwaka wa 2021 wanafunzi wote wa kidato cha nne kufaulu kwa asilimia 100 pia walitoa shukrani kwa Mkurugenzi Mtendaji Kupitia idara ya elimu na Katibu Tawala Mkoa wa Pwani kufanikisha safari hiyo
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.